Psalms 129

Maombi Dhidi Ya Adui Za Israeli

(Wimbo Wa Kwenda Juu)


1 aWamenionea mno tangu ujana wangu;
Israeli na aseme sasa:

2 bwamenionea mno tangu ujana wangu,
lakini bado hawajanishinda.

3 cWakulima wamelima mgongo wangu,
na kufanya mifereji yao mirefu.

4 dLakini Bwana ni mwenye haki;
amenifungua toka kamba za waovu.


5 eWale wote waichukiao Sayuni
na warudishwe nyuma kwa aibu.

6 fWawe kama majani juu ya paa,
ambayo hunyauka kabla hayajakua;

7 gkwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake,
wala akusanyaye kujaza mikono yake.

8 hWale wapitao karibu na wasiseme,
“Baraka ya Bwana iwe juu yako;
tunakubariki katika jina la Bwana.”
Copyright information for SwhKC